Bismillah ar-Rahman ar-Rahim
Iqra Islamic Publications
Welcome to Islam
Accept Islam for your salvation
Live according to Islam for your spiritual progress
QUTB AL-IRSHAD
MAW
LANA AL-HADDAD
Rady Allahu Anhu
(1044 - 1132 A.H)

Kwa jina la Mwenye Ezi Mungu na swala na salamu zimwasilie Wake mkubwa mpenzi pamoja na alize na swahabaze walo azizi. Nani anayemudu zaidi na kuelekea zaidi kumweleza mja wa Mungu wa dhati na kweli isipokuwa mja wa Mungu wa dhati na kweli! Kwa hivyo nani mwengine anayekubalika kumweleza Qutb al-Irshad al-Imam Abdalla bin 'Alawi al-Haddad ila al-Habib 'Ali bin Muhammad al-Habshy, Mungu wape wote radhize, au mtu kama yeye. Na al-Habib 'Ali katika jumla ya aliyoyasema juu ya bwana huyu ni:

Wote waliyofuata twariqa baada yake
wameongozwa na nuru yake iliyozagaa.
Jicho la Tumwa Muhamadi
limetulia juu yake
kwani yeye ni afdhali ya watoto wake.

Nuru inayotajwa hapa ilizaliwa ulimwenguni tarehe tano mwezi wa Safar (mfungo tano) mwaka elfu moja na arubaini na nne katika mji wa Tarim na kwayo al-Imam al-Haddad alipitisha ujana wake kwenye miji ya Tarim, al-Hawi na as-Sabir na akapata malezi mazuri hadi - tafauti kabisa na watoto wa rika lake.

Kwa ufupi yeye ni mmoja katika wale waimamu aliyekusanya tanzu zote na mashina ya utukufu, akatangulia katika ilmu ya ibada zinazomkurubisha mja kwa Mwenye Ezi Mungu wake. Alikuwa na shime ya kulingania watu kwa Mwenye Ezi Mungu hata maimamu wa wakati wake wakamwita Qutb al-Irshad. Katunga vitabu kadha wa kadha, vitabu ambavyo mpaka leo vinadhimishwa na wenye kujua ilmu haswa ndiyo ipi. Ama diwani lake la mashairi, liite bahri na usichelee kuwa utasingiziwa umeitia chumvi.

Shaykh Mohamed Mlamali Adam

< Return