Bismillah ar-Rahman ar-Rahim
Iqra Islamic Publications
Welcome to Islam
Accept Islam for your salvation
Live according to Islam for your spiritual progress

QASAAID


QASIDA ON RAMADAN

IN SWAHILI

Marhaban Yaa Shahru Ramadan

Marhaban Yaa Shahru Ramadan

Marhaban Shahrus Sa’adah wal Ibadah

Marhaban Yaa Shahra Qur’an

Marhaban Yaa Shahra Ghufran

Marhaban Yaa Shahra Burhan wal ‘Ihsan


Bismillahi twaanza
Jina la Mola Muweza
Tupate kuyatimiza
Haya tulo qusudiya

Twa usiya nyoyo zetu
Na walo swahiba zetu
Na Isilamu wenzetu
Akubaliye waswiya

Mwana Adamu sikiya
Yataka kuzingatiya
Inaghururi duniya
Tahadhari na kwambiya

Shikamana na ‘Ibada
Uifanye ndio ‘ada
Utaepukwa na shidda
Na kheri kukujilia

Na swala usiiyate
Kipindi kisikupite
Kwa nguzo na sunna zote
Na sharuti kuzitiya

Mwenye kuwata kuswali
Huwa kafiri wa kweli
Kwa Hadithi ya Rasuli
Sikiya tena sikiya

Na kujifunza ilimu
Ni wajibu Islamu
Mume na mke fahamu
Ujinnga una udhia

Ufunge na Ramadani
Kama ilivyo vyuoni
Siteze teze na Dini
Kwani uta angamia

Kongoni mgeni wetu
Mtukufu Ramadani
Mwezi wa toba jamani
Na baraka na neema

Twakuomba Mawlana
Rabbi tujibu du’ana
Ahali na wetu wana
Twende ziungo zajana

< Return